Di Maria Atua Man United Kwa Pauni Milioni 59.7
Manchester United imekubali kumchukua
Winga wa Real Madrid Anji di maria kwa pauni milioni 59.7 nakuvunja
rekodi ya kiwango cha fedha kwa wachezaji wanaonunuliwa kuchezea timu za
England.
Di Maria mwenye umri wa miaka 26, yuko jijini Manchester na anatarajiwa kufanya vipimo vyake vya kiafya asubuhi hii.
Mchezaji huyo pengine ataungana na
kikosi cha Man United katika mchezo wa ligi kuu ya England utakaofanyika
siku ya jumamosi dhidi ya Burnley Kitita kilichotolewa kwa ajili ya
Muajentina Di Maria kimezidi kiwango cha pauni milioni 50 ambacho
kilitolewa na Chelsea kumnyaka Fernando Torres mwaka 2011.
Manchester United imeshawanunua
wachezaji kama beki wa kushoto Luke Sho,Kiungo wa kati Ander Herrera na
Muajentina Marcos Roho kwa jumla ya Pauni milioni 72 kipindi hiki cha
majira ya joto.
Comments
Post a Comment