Picha 16 za ajali nyingine ya Basi Dodoma leo, alikuwemo pia meneja wa Dr. Cheni
Picha 16 za ajali nyingine ya Basi Dodoma leo, alikuwemo pia meneja wa Dr. Cheni
Aliekuwemo
kwenye hili basi ndio amenitumia hizi picha na kuniambia watu wasiozidi
watano wamefariki dunia wengine zaidi kujeruhiwa baada ya basi lao
kuanguka Mkange Berega.
Basi linaitwa Air Bus na limepata ajali likielekea Dodoma kutokea
Morogo na ni baada ya kifaa cha usukani kushindwa kufanya kazi ambapo
muda mfupi baadae anasema alisikia tu dereva akipiga kelele na kisha
kikafata kishindo, basi likaacha njia na kwenda bondeni.
blog yetu inaendelea
kufatilia ili kupata taarifa kamili ili kujua idadi ya vifo na majeruhi
pamoja na taarifa nyingine ambapo ajali hii imetokea siku tatu baada ya
Waziri wa uchukuzi Dr. Harryson Mwakyembe kufungia kampuni mbili za
mabasi ya J4 Express na Mwanza Coach yaliyogongana na kuua 39 Musoma.
Huyu mama ana watoto Mapacha, hapa alikua analia baada ya kushindwa kumuona mtoto wake mwingine.
Comments
Post a Comment